Saturday, April 27, 2013

SUAREZ AKIRI KOSA NA AMEKATAA KUKATA RUFAA

Nyota wa wekundu wa Anfield Liverpool Luis Suarez amethibitisha kuwa hatakata rufaa kupinga hukumu yake ya kusimamishwa kucheza mechi 10 kwa kosa la kumng`ata kwa meno beki wa Chelsea Branislav Ivanovic, lakini amekiri kukosea na atabadili tabia nje ya uwanja.
Suarez amesema, “Kiukweli nawaomba radhi sana kwa kitendo kile, watu wote niliowaudhi pale Anfield siku hiyo nawaomba wanisamehe sana, lakini kibinafsi namuomba tena msamaha Ivonovic kwa kitendo kile”.
Nyota huyo alisema mambo yote yaliyompata huko England yatamsaidia kubadili tabia yake na kuanzia sasa anataka kujikita kubadili tabia yake na kuwa mchezaji mzuri uwanjani.
All smiles: Suarez was in a cheery mood in training today before his apology appeared on his twitterWakitabasamu: Suarez alionekana mwenye furaha kubwa katika mazoezi ya leo jioni kabla ya kuomba msamaha katika mtandao wake wa Twita.
Suarez aliendelea kueleza kuwa hataki kupotosha ukweli wa kitendo kile kwa kukata rufaa bali amekubali makosa na atatumikia adhabu hiyo kwa moyo mmoja.
Tweet
Suarez

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...