Rais Dk. Jakaya Kikwete (wa pili kulia) Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein, (kulia) Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar Maalim Seif Sharif (wa pili kushoto) na Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi, wakiitikia dua baada ya maziko ya msanii maarufu Fatma Binti Baraka (Bi Kidude) aliyefariki Aprili 17 na kuzikwa Aprili 18 kijijini kwao Kitumba, Wilaya ya Kati Unguja. Picha chini ni Vijana wakiwa wamembeba Bi Kidude wakimsindikiza kwenye makazi yake mapya na sehemu ya Umati wa watu uliokusanyka kumzika Bi Kidude huko Zanzibar.