Thursday, April 25, 2013

WANACHUO WA CHUO CHA UHASIBU ARUSHA WAMTIMUA MKUU WA MKOA

NI BAADA YA KIFO CHA MWANAFUNZI MWENZAO

Wanafunzi wa Chuo cha uhasibu Arusha jana wamemtimua mkuu wa mkoa wa Arusha na kumfanyia fujo kufuatia kwenda kuwatuliza wanafunzi hao baada ya kuanza kuandamana ili waweze kupata taarifa juu ya Umauti uliomkumba mwanafuzni mwenzao Siku ya Jumanne majira ya saa nne usiku katika Eneo la CDA njiro.
Henry Kago alikuwa mwanafunzi wa mwaka wa pili katika Chuo cha Uhasibu aliuwawa usiku wa Jumanne na watu wasiojulikana hivyo wanafunzi hao walijikusanya na kuanza kuandamana kwa Lengo la kupata Taarifa juu ya Umauti uliuomkumba Mwenzao.

Wakiwa katika mipango ya kutaka kuandamana Mbunge wa Arusha Mjini Mh Godless Lema alifika chuoni hapo ilikutaka kujua matatizo yaliyowakumba wanafunzi wa chuo hicho na baadae kidogo ndipo alipofika Mkuu wa Mkoa wa Arusha na kuchafua hali ya hewa katika eneo la chuo hicho na hivyo kusababisha vurugu na fujo kwa mkuu wa mkoa huyo.

kutokana na hali hiyo Jeshi la Polisi lililazimika kutumia nguvu ikiwa pamoja na mabomu ya machozi ili kutuliza ghasia hizo zilizotokea maeneo ya chuo kutokana na uwepo wa Mbunge wa Mjini katika maeneo wanafunzi walipojikusanya kwa lengo la kuandamana kwa amani ili kupata taarifa,Mbunge huyo ameingia katika tuhuma za kuchochea vurugu na fujo chuoni hapo.




Kufuatia vurugu hizo uongozi wa chuo cha uhasibu Arusha kupitia kwa Naibu mkuu wa chuo taaluma Bw.Faraji Kasudi umetangaza kukifunga chuo kwa muda usiojulikana.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...