Saturday, April 27, 2013

SUAREZ AKIRI KOSA NA AMEKATAA KUKATA RUFAA

Nyota wa wekundu wa Anfield Liverpool Luis Suarez amethibitisha kuwa hatakata rufaa kupinga hukumu yake ya kusimamishwa kucheza mechi 10 kwa kosa la kumng`ata kwa meno beki wa Chelsea Branislav Ivanovic, lakini amekiri kukosea na atabadili tabia nje ya uwanja.
Suarez amesema, “Kiukweli nawaomba radhi sana kwa kitendo kile, watu wote niliowaudhi pale Anfield siku hiyo nawaomba wanisamehe sana, lakini kibinafsi namuomba tena msamaha Ivonovic kwa kitendo kile”.
Nyota huyo alisema mambo yote yaliyompata huko England yatamsaidia kubadili tabia yake na kuanzia sasa anataka kujikita kubadili tabia yake na kuwa mchezaji mzuri uwanjani.
All smiles: Suarez was in a cheery mood in training today before his apology appeared on his twitterWakitabasamu: Suarez alionekana mwenye furaha kubwa katika mazoezi ya leo jioni kabla ya kuomba msamaha katika mtandao wake wa Twita.
Suarez aliendelea kueleza kuwa hataki kupotosha ukweli wa kitendo kile kwa kukata rufaa bali amekubali makosa na atatumikia adhabu hiyo kwa moyo mmoja.
Tweet
Suarez

Friday, April 26, 2013

MIKEL RUFFINEL, Mwanamke mwenye makalio makubwa kuliko wote duniani

MWANAMA Mikel Ruffinelli mkazi wa Los Angeles, Marekani, amedhihirisha kuwa ndiye mwanamke mwenye ‘hips’ kubwa zaidi duniani akiwa na mzunguko wa zaidi ya futi 8. Mama huyu wa watoto wanne amekuwa akipata shida kupitisha umbile lake la inchi 100 kwenye mlango na anahitaji nafasi ya watu wawili kwenye ndege. Mikel mwenye umri wa miaka 39 anaendesha magari makubwa kwa vile mwili wake mwenye kilo 190 hauwezi kukaa kwenye magari madogo na anahitaji kiti chenye uimara wa ziada nyumbani.

MWANAMA Mikel Ruffinelli mkazi wa Los Angeles, Marekani, amedhihirisha kuwa ndiye mwanamke mwenye ‘hips’ kubwa zaidi duniani akiwa na mzunguko wa zaidi ya futi 8. Mama huyu wa watoto wanne amekuwa akipata shida kupitisha umbile lake la inchi 100 kwenye mlango na anahitaji nafasi ya watu wawili kwenye ndege. Mikel mwenye umri wa miaka 39 anaendesha magari makubwa kwa vile mwili wake mwenye kilo 190 hauwezi kukaa kwenye magari madogo na anahitaji kiti chenye uimara wa ziada nyumbani

Thursday, April 25, 2013

WANACHUO WA CHUO CHA UHASIBU ARUSHA WAMTIMUA MKUU WA MKOA

NI BAADA YA KIFO CHA MWANAFUNZI MWENZAO

Wanafunzi wa Chuo cha uhasibu Arusha jana wamemtimua mkuu wa mkoa wa Arusha na kumfanyia fujo kufuatia kwenda kuwatuliza wanafunzi hao baada ya kuanza kuandamana ili waweze kupata taarifa juu ya Umauti uliomkumba mwanafuzni mwenzao Siku ya Jumanne majira ya saa nne usiku katika Eneo la CDA njiro.
Henry Kago alikuwa mwanafunzi wa mwaka wa pili katika Chuo cha Uhasibu aliuwawa usiku wa Jumanne na watu wasiojulikana hivyo wanafunzi hao walijikusanya na kuanza kuandamana kwa Lengo la kupata Taarifa juu ya Umauti uliuomkumba Mwenzao.

Wakiwa katika mipango ya kutaka kuandamana Mbunge wa Arusha Mjini Mh Godless Lema alifika chuoni hapo ilikutaka kujua matatizo yaliyowakumba wanafunzi wa chuo hicho na baadae kidogo ndipo alipofika Mkuu wa Mkoa wa Arusha na kuchafua hali ya hewa katika eneo la chuo hicho na hivyo kusababisha vurugu na fujo kwa mkuu wa mkoa huyo.

kutokana na hali hiyo Jeshi la Polisi lililazimika kutumia nguvu ikiwa pamoja na mabomu ya machozi ili kutuliza ghasia hizo zilizotokea maeneo ya chuo kutokana na uwepo wa Mbunge wa Mjini katika maeneo wanafunzi walipojikusanya kwa lengo la kuandamana kwa amani ili kupata taarifa,Mbunge huyo ameingia katika tuhuma za kuchochea vurugu na fujo chuoni hapo.




Kufuatia vurugu hizo uongozi wa chuo cha uhasibu Arusha kupitia kwa Naibu mkuu wa chuo taaluma Bw.Faraji Kasudi umetangaza kukifunga chuo kwa muda usiojulikana.

Borussia Dortmund yaikalisha Real Madrid goli 4 kwa 1


We've done it: Dortmund players celebrate with manager Jurgen Klopp

Vijana wa Dortmund wakishangilia pamoja na meneja wa timu hiyo  Jurgen Klopp










Real
Kiungo wa Real Madrid Christiano Ronaldo, akiwa anatoka nje ya uwanja bila kuamini yaliyotokea

The magic number: Lewandowski shows how many goals he's scored after his hat-trick
Aliyeingarisha Dortmund kwa kufunga magoli yote manne akishabikia goli la 3 huku akonesha ishara kwa vidole.

Wednesday, April 24, 2013

LUIS SUAREZ AFUNGIWA MIAKA 10; NI PIGO JUU YA PIGO KWA MAJOGOO WA JIJI

Mshambuliaji nyota wa Liverpool, Luis Suarez, leo amepewa Adhabu ya Kufungiwa kutocheza Mechi 10 na FA, Chama cha Soka England, kwa Kosa la kumng’ata meno Beki wa Chelsea, Branislav Ivanovic, kwenye Mechi kati ya Liverpool na Chelsea iliyochezwa Jumapili iliyopita.
Katika Mechi hiyo ambayo ilitoka 2-2, Refa Kevin Friend hakuliona tukio hilo lakini Ivanovic alilalamika kwa Refa na kumuonyesha mkono wake ulioumwa.
Mara baada ya Mechi hiyo Suarez aliomba radhi na Klabu ya Liverpool ilimpiga Faini.
Baada ya FA kupata Ripoti ya Refa Friend, ambae alikiri kutoliona tukio hilo, njia ikawa wazi kwa FA kumfungulia Mashitaka Suarez ambae alikiri Kosa lakini aliomba Adhabu yake ibakie Kifungo cha Mechi 3.
Ikitoa Adhabu hiyo, Jopo Huru la FA lilikubali Kifungo cha kawaida cha Mechi 3 kwa Kosa la kuleta vurugu na kuongeza Mechi nyingine 7 kwa kuzingatia uzito wa kosa lenyewe la kinyama.
Adhabu hiyo inaanza mara moja ikimaanisha Suarez atazikosa Mechi zote 4 Liverpool ilizobakisha kwa Msimu huu pamoja na Mechi zao 6 za kwanza za Msimu mpya wa 2013/14 utakaoanza Mwezi Agosti.
Suarez amepewa hadi Ijumaa hii Saa 9 Mchana, Bongo Taimu, kukata Rufaa ikiwa hakuridhika na Adhabu.
I'm back: Luis Suarez returned to training today while the FA deliberated over his punishment for biting
Nimerudi: Luis Suarez akiwa mazoezini leo hii baada ya FC kumfungia mechi 10
Bite club: Suarez sunk his teeth into Branislav Ivanovic during the Premier League match at Anfield
 Suarez akizamisha meno yake katika mkono wa beki wa Chelsea Branislav Ivanovic wakati wa mechi yao ya ligi kuu uwanjani Anfield.
tasty: The bizarre clash was missed by referee Kevin Friend, who had to be told the specifics by Ivanovic
Mwamuzi wa mchezo huo Kevin Friend akiambiwa na Ivanovic kwamba Suarez kaning`ata 
tasty: The bizarre clash was missed by referee Kevin Friend, who had to be told the specifics by Ivanovic
Ivanovic akiwa amkeaa chini kuugulia maumizi ya kung`ata na Surezi.
VIFUNGO VIREFU TOKA FA:
-MIEZI 9: Mchezaji wa Manchester United Eric Cantona kwa kumpiga Mshabiki Mwaka 1995
-MIEZI 9: Kipa wa Chelsea Mark Bosnich kwa kugundulika kutumia Kokeni Mwaka 2003
-MIEZI 8: Rio Ferdinand wa Manchester United kwa kukosa kupimwa utumiaji Madawa yanayokatazwa hapo Mwaka 2003
-MECHI 12: Joey Barton wa QPR kwa kuleta vurugu kwenye Mechi na Man City Mwaka 2012.
-MECHI 11: Paolo Di Canio alipokuwa Sheffield Wednesday kwa kumsukuma Refa Paul Alcock Mwaka 1998
-MECHI 10: David Prutton wa Southampton kwa kumsukuma Refa Alan Wiley Mwaka 2005
-MECHI 10: Luis Suarez kwa kumuuma Branislav Ivanovic Mwaka 2013
-MECHI 9: Paul Davis wa Arsenal kwa kumpiga ngumi Glenn Cockerill wa Southampton Mwaka 1988 na kumvunja taya.
-MECHI 8: Luis Suarez kwa kumkashifu Kibaguzi Patrice Evra Mwaka 2011
-MECHI 8: Ben Thatcher wa Man City kwa kumpiga kipepsi Pedro Mendes wa
Portsmouth Mwaka 2006.
-MECHI 5: Roy Keane wa Man United kwa kuandika maneno yasiyokubalika kwenye Kitabu chake hapo Mwaka 2002

Sunday, April 21, 2013

MKWAWA YAiFUNIKA TUMAINI KWENYE MASHINDANO YA GRAND MALTA

 
 Chuo cha Tumaini kikichuana na Chuo cha Mkwawa ambapo Tumaini ilifungwa set 3 kwa 1

                                Timu ya wasichana ya mpira wa pete ya Mkwawa (nyekundu) ikichuana na timu ya chuo cha Tumaini katika tamasha la Grand Malta na kufanikiwa kuifunga 23 kwa 18

                                  KISHA IKAWADIA ZAMU YA BURUDANI YA MUZIKI


                                          Dj Choka akiwa katika pozi na aliyekuwa waziri wa michezo na burudani wa chuo kikuu cha Iringa Lazaro Mlyuka


                                  Baadhi ya mashabiki wakiwa wanamshabikia Joh Makini baada ya kupanda stejini.

WAMILIKI WA DALADALA BADO WANAMAKA HAWAJARIDHIKA NA NAULI KUPANDISWA

WALALAMIKA NAULI HAZITOSHI: WANADAI INABIDI ZIONGEZWE,

d
WAKATI wananchi wakilalamika kupanda kwa nauli kuwa kumeongeza ugumu wa maisha, Mwenyekiti wa Chama cha wamiliki wa Daladala, Sabri Mabrouk amesema bado nauli hiyo ni kiduchu.
Mabrouk aliyasema hayo jijini Dar es Salaam jana, kuwa wananchi wanapaswa kutambuwa kuwa ugumu wa maisha haukuanza leo.
 Alisema hali hiyo haikusababishwa na kupanda kwa nauli bali ulikuwepo tangu utawala wa awamu ya kwanza na utaendelea kuwepo katika tawala mbalimbali zitakazokuja.
 “Kwa watu tulioishi katika maisha ya ugumu ugumu ni kisema hivyo wananielewa lakini najua wapo ambao wamenufaika kutokana na kuwa na jamaa ambao walikuwa viongozi katika serikali hao labda ndio wanaweza kushindwa kujua ugumu wa maisha katika nchi hii.
“pia wananchi wajue kila kitu kizuri kina gharama zake hivyo ili kuboresha huduma zetu za usafiri ni lazima wananchi wakubali kuchangia kile kinachostahili” .”alisema Mbrouk.
 Akizungumzia mfumo wa huduma ya usafirishaji jijini kuwa wa kapuni, Mabrouk, alisema haukwepiki bali ni mhuhimu kwa wamiliki wa daladala kutumia fursa hiyo kujiunga na kuanzisha kampuni.
 Aliwataka wamiliki wenzake kuacha kuwasikiliza baadhi ya watu wanaotaka kuwapotosha kuwa mpango huo haulengi kuwanufaisha wao bali kuna wahusika maalum.
 Mabrouk alisema mfumo huo umewalenga wamiliki wa daladala kwanza, endapo watadharau basi fursa hiyo itakwenda kweli kwa wengine.
 “Kutakuwa na kampuni mbili kwa kuanzia zitakazo simamia huduma hiyo ya usafiri moja yadi yake yakuweka magari itakuwa Jangwani na nyingine itakuwa katika Kituo cha Mabasi yaendayo mikoani na nje ya nchi”alisema Mbrouk.

HATIMAYE DNA AFANYA NGOMA NA MR. NICE(download hapo chini)


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...