Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom
Tanzania, Kelvin Twissa akiongea kwa simu na Mshindi wa Droo ya mwishi ya
“MAHELA “Bw.Valelian Nickodemus(22) wa Mkoa wa Kigoma aliyejishindia shilingi
Milioni 100.
MSHINDI WA MILIONI 100 APATIKANA
Hatimaye Mshindi wa Milioni 100 wa
Promosheni ya Vodacom Mahela amepatikana ikishuhudia Mwanafunzi chuo cha
Ualimu cha Mkoani Kigoma Bw.Valelian Nickodemus(22) akiibuka mshindi
kupitia droo kubwa iliyochezeshwa leo jumatatu.
Mshindi huyo amepatikana miongoni mwa
mamilioni ya washiriki walioshiriki kucheza katika promosheni hiyo,
Katika mahojiano yaliyofanyika kwa njia ya simu Mshindi huyo ameishukuru
kampuni ya Vodacom kwa kumuwezesha kushinda kiasi hiko kwani hayakuwa
mategemeo yake katika maisha yake.
"Watu wengi hawakuwa wanaamini kuwa
Promosheni hizi ni za kweli, Sikuwa na pesa ya kucheza moja kwa moja
katika Promosheni hii ila nilipotumiwa pesa ya matumizi na mzee niliamua
kuweka na kushiriki katika Promosheni hii, Hakika nimefurahi sana na
ninawashukuru Vodacom, alisema Nickodemus.
Kwa upande wake mkuu wa kitengo cha
Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa amewapongeza
Wateja wa mtandao huo kwa kushiriki katika promosheni hiyo na kumpongeza
kwa upekee mshindi wa Promosheni hiyo na kujinasibu kuwa anajivunia
mafanikio ambayo Promosheni hiyo imeyapata kwa kufanikiwa kubadili
maisha ya mamia ya Watanzania.
"Sisi kama Vodacom tumefurahi kwa
kumpata mshindi wetu wa mwisho ambaye ameibuka kidedea kati ya Mamilioni
ya Watanzania lazima tukiri kuwa ni bahati kubwa na tunatoa pongezi za
kipekee kwa mshindi wetu, alisema Twissa na kuongeza kuwa\
"Zaidi ya yote tunajivunia kwa upekee
kabisa namna ambavyo promosheni hii imebadilisha mamia ya maisha ya
Watanzania, Tumepata washindi kutoka katika Nyanja mbalimbali wakiwemo
wakulima, wafanya biashara ndogondogo wanafunzi pamoja na wastaafu wengi
ambao nao wameendelea kuboresha maisha yao.
Tangu Promosheni ya MAHELA kuzinduliwa
tarehe 24 Mwezi wa kwanza na washindi 333 wamepatikana na kushuhudia
kiasi cha Shilingi milioni 480 zikitolewa hadi sasa.
No comments:
Post a Comment