Wednesday, April 24, 2013

LUIS SUAREZ AFUNGIWA MIAKA 10; NI PIGO JUU YA PIGO KWA MAJOGOO WA JIJI

Mshambuliaji nyota wa Liverpool, Luis Suarez, leo amepewa Adhabu ya Kufungiwa kutocheza Mechi 10 na FA, Chama cha Soka England, kwa Kosa la kumng’ata meno Beki wa Chelsea, Branislav Ivanovic, kwenye Mechi kati ya Liverpool na Chelsea iliyochezwa Jumapili iliyopita.
Katika Mechi hiyo ambayo ilitoka 2-2, Refa Kevin Friend hakuliona tukio hilo lakini Ivanovic alilalamika kwa Refa na kumuonyesha mkono wake ulioumwa.
Mara baada ya Mechi hiyo Suarez aliomba radhi na Klabu ya Liverpool ilimpiga Faini.
Baada ya FA kupata Ripoti ya Refa Friend, ambae alikiri kutoliona tukio hilo, njia ikawa wazi kwa FA kumfungulia Mashitaka Suarez ambae alikiri Kosa lakini aliomba Adhabu yake ibakie Kifungo cha Mechi 3.
Ikitoa Adhabu hiyo, Jopo Huru la FA lilikubali Kifungo cha kawaida cha Mechi 3 kwa Kosa la kuleta vurugu na kuongeza Mechi nyingine 7 kwa kuzingatia uzito wa kosa lenyewe la kinyama.
Adhabu hiyo inaanza mara moja ikimaanisha Suarez atazikosa Mechi zote 4 Liverpool ilizobakisha kwa Msimu huu pamoja na Mechi zao 6 za kwanza za Msimu mpya wa 2013/14 utakaoanza Mwezi Agosti.
Suarez amepewa hadi Ijumaa hii Saa 9 Mchana, Bongo Taimu, kukata Rufaa ikiwa hakuridhika na Adhabu.
I'm back: Luis Suarez returned to training today while the FA deliberated over his punishment for biting
Nimerudi: Luis Suarez akiwa mazoezini leo hii baada ya FC kumfungia mechi 10
Bite club: Suarez sunk his teeth into Branislav Ivanovic during the Premier League match at Anfield
 Suarez akizamisha meno yake katika mkono wa beki wa Chelsea Branislav Ivanovic wakati wa mechi yao ya ligi kuu uwanjani Anfield.
tasty: The bizarre clash was missed by referee Kevin Friend, who had to be told the specifics by Ivanovic
Mwamuzi wa mchezo huo Kevin Friend akiambiwa na Ivanovic kwamba Suarez kaning`ata 
tasty: The bizarre clash was missed by referee Kevin Friend, who had to be told the specifics by Ivanovic
Ivanovic akiwa amkeaa chini kuugulia maumizi ya kung`ata na Surezi.
VIFUNGO VIREFU TOKA FA:
-MIEZI 9: Mchezaji wa Manchester United Eric Cantona kwa kumpiga Mshabiki Mwaka 1995
-MIEZI 9: Kipa wa Chelsea Mark Bosnich kwa kugundulika kutumia Kokeni Mwaka 2003
-MIEZI 8: Rio Ferdinand wa Manchester United kwa kukosa kupimwa utumiaji Madawa yanayokatazwa hapo Mwaka 2003
-MECHI 12: Joey Barton wa QPR kwa kuleta vurugu kwenye Mechi na Man City Mwaka 2012.
-MECHI 11: Paolo Di Canio alipokuwa Sheffield Wednesday kwa kumsukuma Refa Paul Alcock Mwaka 1998
-MECHI 10: David Prutton wa Southampton kwa kumsukuma Refa Alan Wiley Mwaka 2005
-MECHI 10: Luis Suarez kwa kumuuma Branislav Ivanovic Mwaka 2013
-MECHI 9: Paul Davis wa Arsenal kwa kumpiga ngumi Glenn Cockerill wa Southampton Mwaka 1988 na kumvunja taya.
-MECHI 8: Luis Suarez kwa kumkashifu Kibaguzi Patrice Evra Mwaka 2011
-MECHI 8: Ben Thatcher wa Man City kwa kumpiga kipepsi Pedro Mendes wa
Portsmouth Mwaka 2006.
-MECHI 5: Roy Keane wa Man United kwa kuandika maneno yasiyokubalika kwenye Kitabu chake hapo Mwaka 2002

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...