Photos by John Bukuku
Monday, April 22, 2013
SERIKALI YAPOKEA DOLA ZA KIMAREKANI BILIONI 16 KUSAIDIA MRADI WA MAJI
Serikali ya Tanzania yasaini mkataba wa jumla ya dola za
kimarekani milioni 16 kusaidia mradi wa maji Orkesumet mkoani Manyara. Mkataba
huo umesainiwa kati ya Serikali ya Tanzania na OPEC Fund For International
Development (OFID) wakishirikiana na BADEA. OPEC wametoa milioni 8 na BADEA
wametoa milioni 8. Ili kufanikisha mradi huu Serikali ya Tanzania itatoa dola
za kimarekali milioni 2.42, Hivyo kufanya mradi huu kufikia jumla ya dola za
Kimarekani milioni 18.42.
Waziri wa Fedha Dkt. Wiliam Mgimwa akisaini
mkataba wa maji ambao utawasaidia wananchi ya Manyara.
Mkurugenzi Mkuu wa
OFID (OPEC Fund For International Development Bw. Suleiman Al-Herbish
akishauriana na Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Wiliam Mgimwa kabla ya kusaini mkataba
wa mradi wa maji.
Mkurugenzi Mkuu wa
OFID (OPEC Fund For International Development Bw. Suleiman Al-Herbish
akishauriana na Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Wiliam Mgimwa kabla ya kusaini mkataba
wa mradi wa maji.
Waziri wa Fedha Mhe.
Dkt. Wiliam Mgimwa akibadilishana mkataba na Mkurugenzi wa OFID kushoto ni
Katibu wa Waziri wa Fedha Bw. Omar Khama akiwasikiliza wafanyakazi wa
OFID.
Waziri wa Fedha
Dkt Wiliam Mgimwa akipokea mkataba kutoka kwa mchumi wa Wizara ya Fedha Bw.
Patrck Pima.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment