Sunday, April 21, 2013

WAMILIKI WA DALADALA BADO WANAMAKA HAWAJARIDHIKA NA NAULI KUPANDISWA

WALALAMIKA NAULI HAZITOSHI: WANADAI INABIDI ZIONGEZWE,

d
WAKATI wananchi wakilalamika kupanda kwa nauli kuwa kumeongeza ugumu wa maisha, Mwenyekiti wa Chama cha wamiliki wa Daladala, Sabri Mabrouk amesema bado nauli hiyo ni kiduchu.
Mabrouk aliyasema hayo jijini Dar es Salaam jana, kuwa wananchi wanapaswa kutambuwa kuwa ugumu wa maisha haukuanza leo.
 Alisema hali hiyo haikusababishwa na kupanda kwa nauli bali ulikuwepo tangu utawala wa awamu ya kwanza na utaendelea kuwepo katika tawala mbalimbali zitakazokuja.
 “Kwa watu tulioishi katika maisha ya ugumu ugumu ni kisema hivyo wananielewa lakini najua wapo ambao wamenufaika kutokana na kuwa na jamaa ambao walikuwa viongozi katika serikali hao labda ndio wanaweza kushindwa kujua ugumu wa maisha katika nchi hii.
“pia wananchi wajue kila kitu kizuri kina gharama zake hivyo ili kuboresha huduma zetu za usafiri ni lazima wananchi wakubali kuchangia kile kinachostahili” .”alisema Mbrouk.
 Akizungumzia mfumo wa huduma ya usafirishaji jijini kuwa wa kapuni, Mabrouk, alisema haukwepiki bali ni mhuhimu kwa wamiliki wa daladala kutumia fursa hiyo kujiunga na kuanzisha kampuni.
 Aliwataka wamiliki wenzake kuacha kuwasikiliza baadhi ya watu wanaotaka kuwapotosha kuwa mpango huo haulengi kuwanufaisha wao bali kuna wahusika maalum.
 Mabrouk alisema mfumo huo umewalenga wamiliki wa daladala kwanza, endapo watadharau basi fursa hiyo itakwenda kweli kwa wengine.
 “Kutakuwa na kampuni mbili kwa kuanzia zitakazo simamia huduma hiyo ya usafiri moja yadi yake yakuweka magari itakuwa Jangwani na nyingine itakuwa katika Kituo cha Mabasi yaendayo mikoani na nje ya nchi”alisema Mbrouk.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...